Posts

Showing posts from December, 2022

Halmashauri ya Wilaya Tarime imekamilisha kwa wakati na ubora ujenzi wa vyumba vya madarasa 23 vyenye thamani ya Tshs milioni 460.

Image
Akifafanua wakati wa ukaguzi miradi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndugu Solomon I Shati ameeleza kuwa fedha hizi ni kutoka serikali kuu hivyo alimshukuru Mh. Dr Samia Suluhu Hasan kwa kuleta fedha hizo zenye lengo la kuboresha mazingira mazuri ya kujifunzia na kujisomea kwa wanafunzi hivyo kuinua ufauru wa wanafunzi. Madarasa hayo yana uwezo wa kubeba au kuchukua wanafuzi wa kutosha hivyo kufanikisha adhma ya kuchukua wanafunzi wengi wa shule ya msingi waliofauru mwaka huu 2022. Akifanunua zaidi alieleza kuwa pamoja na changamoto ya kupanda kwa vifaa bado wamefanikiwa kukamilisha katika ubora, hivyo ametoa wito kwa wazazi kuleta wanafunzi katika shule walizopangwa kwa wakati.

MKUU WA WILAYA YA TARIME AONGONZA KUFANYA USAFI KUADHIMISHA MIAKA 61 YA UHURU WA TANZANIA BARA

Image
Mkuu wa Wilaya ya Tarime Mheshimiwa Col. Michael Mntenjele leo amewaongoza viongozi na wananchi katika kufanya usafi katika mji wa Sirari maeneo ya soko, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Kauli Mbiu: MIAKA 61 YA UHURU AMANI NA UMOJA NI NGUZO YA MAENDELEO YETU  
Image
Siku ya leo tarehe 8 Disemba 2022 Mkurugenzi Mtendaji  Ndugu Solomon I. Shati, watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Tarime na wananchi  wa sirari kwa pamoja wameshiriki zoezi la kufanya usafi katika mji wa Sirari maeneo ya soko, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Kauli Mbiu: MIAKA 61 YA UHURU AMANI NA UMOJA NI NGUZO YA MAENDELEO YETU