Posts

NAIBU WAZIRI TAMISEMI MHE. Dkt. FESTO JOHN DUGANGE (MB) AMEIPONGEZA HALMASHAURI YA WILAYA TARIME KWA UJENZI WA SHULE MPYA YA BUKIRA

Naibu waziri TAMISEMI Mhe. Dr Festo John Dugange (Mb) ameipongeza Halmashauri ya Wilaya Tarime kwa ujenzi wa shule mpya ya Bukira iliyopo Kata ya Sirari iliyogharimu shilingi milioni 470 fedha toka Serikali kuu, aidha amesifu ubora wa ujenzi uliozingatia thamani ya fedha tayari kupokea wanafunzi mapema 2023

Halmashauri ya Wilaya Tarime imekamilisha kwa wakati na ubora ujenzi wa vyumba vya madarasa 23 vyenye thamani ya Tshs milioni 460.

Image
Akifafanua wakati wa ukaguzi miradi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndugu Solomon I Shati ameeleza kuwa fedha hizi ni kutoka serikali kuu hivyo alimshukuru Mh. Dr Samia Suluhu Hasan kwa kuleta fedha hizo zenye lengo la kuboresha mazingira mazuri ya kujifunzia na kujisomea kwa wanafunzi hivyo kuinua ufauru wa wanafunzi. Madarasa hayo yana uwezo wa kubeba au kuchukua wanafuzi wa kutosha hivyo kufanikisha adhma ya kuchukua wanafunzi wengi wa shule ya msingi waliofauru mwaka huu 2022. Akifanunua zaidi alieleza kuwa pamoja na changamoto ya kupanda kwa vifaa bado wamefanikiwa kukamilisha katika ubora, hivyo ametoa wito kwa wazazi kuleta wanafunzi katika shule walizopangwa kwa wakati.

MKUU WA WILAYA YA TARIME AONGONZA KUFANYA USAFI KUADHIMISHA MIAKA 61 YA UHURU WA TANZANIA BARA

Image
Mkuu wa Wilaya ya Tarime Mheshimiwa Col. Michael Mntenjele leo amewaongoza viongozi na wananchi katika kufanya usafi katika mji wa Sirari maeneo ya soko, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Kauli Mbiu: MIAKA 61 YA UHURU AMANI NA UMOJA NI NGUZO YA MAENDELEO YETU  
Image
Siku ya leo tarehe 8 Disemba 2022 Mkurugenzi Mtendaji  Ndugu Solomon I. Shati, watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Tarime na wananchi  wa sirari kwa pamoja wameshiriki zoezi la kufanya usafi katika mji wa Sirari maeneo ya soko, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Kauli Mbiu: MIAKA 61 YA UHURU AMANI NA UMOJA NI NGUZO YA MAENDELEO YETU  

TAMISEMI YARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI MADARASA TARIME VIJIJINI,NAIBU WAZIRI DAVID SILINDE ATOA PONGEZI ZA DHATI

Image
 Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI- Elimu, David Silinde leo Novemba 27, 2022 amekagua maendeleo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ya shule za sekondari katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime mkoani Mara na kutaka kasi aliyoikuta iendelee ili yakamilike kwa wakati. “Ninatoa rai kasi hii iendelee, madarasa yote katika halmashauri hii yakamilike kwa wakati na mtoe taarifa mkoani ili nao watuletee, kwa sababu na sisi tuna lengo la kumkabidhi Rais madarasa yote 8,000 yakiwa yamekamilika,” Silinde alisema mara baada ya kukagua ujenzi wa madarasa mawili katika Shule ya Sekondari Nyantira. Amesema yupo katika ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa maeneo mbalimbali nchini, kutokana na fedha zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ili kuwezesha wanafunzi wote watakaochaguliwa kuingia kidato cha kwanza mwaka 2023 wanapata nafasi. “Rais ametoa fedha za madarasa 8,000 nchini ili watoto wote wapate nafasi kama alivyofanya mwaka jan

MBUNGE WA TARIME VIJIJINI AWATUA WANANCHI WAKE MZIGO WA MICHANGO KWA KUTOA MIFUKO YA SIMENTI 660.

Image
Mhe. Mwita Waitara Naibu Waziri Ofisi Makamu wa Rais Muungano na Mazingira(Mbunge), ametoa mifuko ya simenti 660 katika miradi ya shule za sekondari na msingi. Hivyo kupelekea shule  8 za halmashauri ya wilaya Tarime mkoani Mara kunufaika na mifuko ya sementi iliyotolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais muungano na mazingira Mwita Mwikwabe Waitara. Akikabidhi mifuko hiyo katika shule mbalimbali kwa nyakati tofauti Waitara alisema kuwa kufanya hivyo ni kuhakikisha shule zinajengwa na kukamilika ili kuondolea wanafunzi kutembea mwendo mrefu wakifuata masomo. “Shule zinapokuwa karibu zinasaidia kupunguza umbali wa wanafunzi kutembea mwendo mrefu wakutembea kufuata  masomo shule za mbali ikiwemo kupunguza mimba mashuleni kwa watoto wa kike”alisema Waitara. Waitara aliongeza kusema kuwa kipindi cha uongozi wa awamu ya Tano chini ya Rais wake John Pombe Magufuli serikali imedhamiria kuwafikishia wananchi huduma karibu na kuwaondolea adha za muda mrefu kama vile Afya,Elimu,M

Jeshi la Kujenga Taifa Tayari wametoa Majina ya waliyochaguliwa kujiuunga

Image