Posts

Showing posts from March, 2021

MBUNGE WA TARIME VIJIJINI AWATUA WANANCHI WAKE MZIGO WA MICHANGO KWA KUTOA MIFUKO YA SIMENTI 660.

Image
Mhe. Mwita Waitara Naibu Waziri Ofisi Makamu wa Rais Muungano na Mazingira(Mbunge), ametoa mifuko ya simenti 660 katika miradi ya shule za sekondari na msingi. Hivyo kupelekea shule  8 za halmashauri ya wilaya Tarime mkoani Mara kunufaika na mifuko ya sementi iliyotolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais muungano na mazingira Mwita Mwikwabe Waitara. Akikabidhi mifuko hiyo katika shule mbalimbali kwa nyakati tofauti Waitara alisema kuwa kufanya hivyo ni kuhakikisha shule zinajengwa na kukamilika ili kuondolea wanafunzi kutembea mwendo mrefu wakifuata masomo. “Shule zinapokuwa karibu zinasaidia kupunguza umbali wa wanafunzi kutembea mwendo mrefu wakutembea kufuata  masomo shule za mbali ikiwemo kupunguza mimba mashuleni kwa watoto wa kike”alisema Waitara. Waitara aliongeza kusema kuwa kipindi cha uongozi wa awamu ya Tano chini ya Rais wake John Pombe Magufuli serikali imedhamiria kuwafikishia wananchi huduma karibu na kuwaondolea adha za muda mrefu kama vile Afya,Elimu,M