Halmashauri ya Wilaya Tarime imekamilisha kwa wakati na ubora ujenzi wa vyumba vya madarasa 23 vyenye thamani ya Tshs milioni 460.

Akifafanua wakati wa ukaguzi miradi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndugu Solomon I Shati ameeleza kuwa fedha hizi ni kutoka serikali kuu hivyo alimshukuru Mh. Dr Samia Suluhu Hasan kwa kuleta fedha hizo zenye lengo la kuboresha mazingira mazuri ya kujifunzia na kujisomea kwa wanafunzi hivyo kuinua ufauru wa wanafunzi. Madarasa hayo yana uwezo wa kubeba au kuchukua wanafuzi wa kutosha hivyo kufanikisha adhma ya kuchukua wanafunzi wengi wa shule ya msingi waliofauru mwaka huu 2022. Akifanunua zaidi alieleza kuwa pamoja na changamoto ya kupanda kwa vifaa bado wamefanikiwa kukamilisha katika ubora, hivyo ametoa wito kwa wazazi kuleta wanafunzi katika shule walizopangwa kwa wakati.

Comments

Popular posts from this blog

Mkuu wa Mkoa wa Mara Awapongeza Halmashauri ya Wilaya ya Tarime