TAMISEMI YARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI MADARASA TARIME VIJIJINI,NAIBU WAZIRI DAVID SILINDE ATOA PONGEZI ZA DHATI
Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI- Elimu, David Silinde leo Novemba 27, 2022 amekagua maendeleo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ya shule za sekondari katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime mkoani Mara na kutaka kasi aliyoikuta iendelee ili yakamilike kwa wakati.
“Ninatoa rai kasi hii iendelee, madarasa yote katika
halmashauri hii yakamilike kwa wakati na mtoe taarifa mkoani ili nao watuletee,
kwa sababu na sisi tuna lengo la kumkabidhi Rais madarasa yote 8,000 yakiwa
yamekamilika,” Silinde alisema mara baada ya kukagua ujenzi wa madarasa mawili
katika Shule ya Sekondari Nyantira.
Amesema yupo katika ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa
vyumba vya madarasa maeneo mbalimbali nchini, kutokana na fedha zilizotolewa na
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ili kuwezesha
wanafunzi wote watakaochaguliwa kuingia kidato cha kwanza mwaka 2023 wanapata
nafasi.
“Rais ametoa fedha za madarasa 8,000 nchini ili watoto wote
wapate nafasi kama alivyofanya mwaka jana [2021],” Naibu Waziri David Silinde
amesema na kuwataka viongozi husika kuhakikisha yanakamilika kwa wakati.
Comments
Post a Comment