MBUNGE WA TARIME VIJIJINI AWATUA WANANCHI WAKE MZIGO WA MICHANGO KWA KUTOA MIFUKO YA SIMENTI 660.




Mhe. Mwita Waitara Naibu Waziri Ofisi Makamu wa Rais Muungano na Mazingira(Mbunge), ametoa mifuko ya simenti 660 katika miradi ya shule za sekondari na msingi.

Hivyo kupelekea shule  8 za halmashauri ya wilaya Tarime mkoani Mara kunufaika na mifuko ya sementi iliyotolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais muungano na mazingira Mwita Mwikwabe Waitara.

Akikabidhi mifuko hiyo katika shule mbalimbali kwa nyakati tofauti Waitara alisema kuwa kufanya hivyo ni kuhakikisha shule zinajengwa na kukamilika ili kuondolea wanafunzi kutembea mwendo mrefu wakifuata masomo.

“Shule zinapokuwa karibu zinasaidia kupunguza umbali wa wanafunzi kutembea mwendo mrefu wakutembea kufuata  masomo shule za mbali ikiwemo kupunguza mimba mashuleni kwa watoto wa kike”alisema Waitara.

Waitara aliongeza kusema kuwa kipindi cha uongozi wa awamu ya Tano chini ya Rais wake John Pombe Magufuli serikali imedhamiria kuwafikishia wananchi huduma karibu na kuwaondolea adha za muda mrefu kama vile Afya,Elimu,Maji na miundombinu ya barabara.



Naye mwenyekiti wa halmashauri ya Tarime vijijini,Simion Kiles Samwel aliwahakikishia wananchi kuwa atahakikisha anasimamia maendeleo yao kwa dhati, pamoja na kumpongeza mbunge Mhe Mwenyekiti alichangia kiasi cha shilingi laki tano na mifuko thelathini ya saruji.

Comments

Popular posts from this blog

Mkuu wa Mkoa wa Mara Awapongeza Halmashauri ya Wilaya ya Tarime