MAAGIZO YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, DKT. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI ALIYOYATOA WAKATI WA ZIARA YAKE WILAYANI TARIME YATEKELEZWA KWA KISHINDO
Hatimaye Wakazi 1,639 wa Vijiji vya Matongo na Nyabichune
katika eneo la Nyamongo Wilayani Tarime Mkoa wa Mara wamelipwa fidia ya jumla
ya Shilingi Bilioni 33 baada ya kusubiri kwa kipindi cha miaka 10.
Fidia hiyo imelipwa Mei 20, 2020 na Mgodi wa Barrick North Mara ikiwa
Utekelezaji wa Maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Magufuli aliyoyatoa wakati wa ziara yake Wilayani Tarime ambapo alitaka suala hilo ikiwemo la uchafuzi
wa mazingira yamalizwe haraka.
Akizungumza wakati wa Ufunguzi wa utoaji fidia na Ugawaji wa Cheki kwa Wakazi hao waliopisha
maeneo yao kwa ajili ya uendelezaji wa shughuli za mgodi huo, Waziri wa Madini
Doto Biteko amewahakikishia wote wenye haki ya kulipwa fidia hiyo kuwa
watalipwa fedha zao.
Aidha, ametoa pongeza kwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi na kueleza kuwa Wizara hiyo ilifanya kazi usiku na mchana
kuhakikisha inamaliza mgogoro wa fidia uliokuwepo baina ya wananchi na mgodi
huo.
Comments
Post a Comment