Mkuu wa Mkoa wa Mara Awapongeza Halmashauri ya Wilaya ya Tarime
Tarime inapendeza
MKUU WA
MKOA WA MARA AWAPONGEZA HALMASHAURI YA WILAYA YA TARIME KWA KUTII AGIZO HARAKA LA
MHE DK. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFURI RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KWA
KUHAMIA NYAMWANGA.
Kufuatia agizo la Rais wa awamu ya tano Dk.John Pombe Joseph Magufuri kuagiza
halmashauri zote kuhama mjini na kwenda maeneo ya vijijini (maeneo yao ya utawala), alipokuwa
katika ziara ya kikazi mkoani Rukwa katika wilaya ya sumbawanga mji mdogo
wa Lahela ili kuhakikisha wanatoa huduma kwa wananchi wanyonge.
Naye
mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya tarime Ndugu. Apoo Castro Tindwa kwa
kushirikiana na madiwani wa halmashauli hiyo wameafikiana kuhama haraka kutoka
katika halmashauri ya mji wa Tarime na kwenda katika eneo lililopangwa kwa
ajili ya halmashauri hiyo ikiwa ni kati ya halmashauri 31 ambazo azipo katika
maeneo ya kiutawala.
Hata
hivyo halmashauri ya wilaya ya Tarime tayari imeshahamia katika kijiji cha
Nyamwaga Kata ya Nyamwaga ndani ya majengo ya ofisi ya tarafa na kijiji kwa
muda, wakisubiria kujengwa kwa ofisi zake katika eneo lililotengwa kwa ajili ya
makao makuu ya Halmashauri ya wilaya Tarime Nyamwaga.
Katika
ziara yake ya kutembelea na kukagua makao mapya ya Halmashauri ya wilaya ya
Tarime Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Adam Malima amewapongeza halmashauri ya wilaya
ya Tarime kwa kutii agizo la Mhe DK. John Pombe Joseph Magufuri Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania kwa kuhamia Nyamwanga na kuhakikisha wanatoa huduma kwa
wananchi wanyonge,
Wakati
wa kikao chake na waheshimiwa madiwani na wakuu wa idara kilichofanyika katika Ukumbi
wa shule ya Sekondari JK Nyerere iliyopo Nyamwaga, Mhe. Adam Malima aliwapatia
nafasi waheshiwa madiwani kutoa maoni juu ya hatua ya baadhi ya kata za
halmashauri ya wilaya ya Tarime kuhamia Halmashauri ya mji wa Tarime, Katika
maoni yao waheshimiwa madiwani walimpongeza Mkuu wa Mkoa Mara kwa wazo la kuhamisha
kata nane (8) za Sirari,Regicheri,Mwema,Susuni,Bumera,Komaswa,Manga na Kiore
kwa lengo la kuwaondolea wananchi wanyonge adha ya umbali wa kufuata huduma
makao makuu ya halmashauri ya wilaya ya Tarime yaliyopo Nyamwaga kufuatia
jogorafia iliyopo.
Comments
Post a Comment