Baraza la madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Tarime limeipongeza Halmashauri kwa kuweza kupata hati safi katika hesabu za serikali za mwaka wa fedha 2017/2018 tarehe 04/07/2019 katika ukumbi wa halmashauri.

Halmashauri  www.tarimedc.go.tzya wilaya ya Tarime kupitia Baraza la Madiwani la kupokea na kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali. Kwa mara nyingine Halmashauri  ya wilaya ya Tarime imeweza kupata hati safi kwa mwaka wa fedha 2017/2018, wakipokea hati hiyo  kwa niaba ya wananchi wa Halmashauri ya wilaya ya Tarime wakati wa mkutano uliofanyika tarehe 4/7/2019 katika ukumbi wa Halmashauri.

Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Tarime limeipongeza Halmashauri kwa kupata Hati safi baada ya Mkurugenzi wa  Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Bw.Apoo C. Tindwa kutoa taarifa ya kupokea ripoti kutoka kwa Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG )inayoonesha Halmashauri kuwa na hati safi kwa mwaka wa fedha 2017/2018. 

  Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Tarime Mhe.Moses Misiwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao hicho aliipongeza Halmashauri kwa kupata hati safi katika hesabu za jumla, akisema kuwa takribani kwa miaka mitatu mfululizo halmashauri imeweza kupata hati safi kwa kipindi cha awamu hii ya tano. 
UFUATAO NI MFULULIZO WA HATI ZA UKAGUZI WA HESABU ZA JUMLA ZA HALMASHAURI YA WILAYA YA TARIME KATIKA KIPINDI CHA MIAKA MITATU:-
2015/162016/172017/18
SafiSafiSafi


Comments

Popular posts from this blog

Mkuu wa Mkoa wa Mara Awapongeza Halmashauri ya Wilaya ya Tarime