KAMATI YA BUNGE YAPONGEZA UJENZI KITUO CHA AFYA MURIBA.
www.tarimedc.go.tz
Kamati ya Bunge ya hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) imepongeza
ujenzi wa kituo cha Afya Muriba pamoja na huduma zinazotolewa pale ambapo
imeitaka Halmashauri ya wilaya ya Tarime kuendelea kutumia Vyema Mapato yake ya
Ndani huku ikitekeleza vyema Miradi ya Maji, Afya , Elimu na Barabara ili
kutatu changamoto za Wananchi.
Kauli hiyo imetolewa na Mhe:
Abdallah Chikota ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo kipindi
walipotembelea kituo cha Afya Muriba kwa ajili ya kukagua Miradi hiyo.
“Sisi kama Kamati tumejilidhisha
pia tunafurahishwa na huduma zinazotolewa hapa na changamoto ambazo zinakumba
hiki kituo cha Afya tutaenda kuangalia kwenye vitabu kama zimewekwa ili
kuzisemea kwa lengo la kuzitatu” alisema Chikota.
Kwa Upande Wake Naibu waziri wa
Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe: Mwita Waitara naye alipongeza Wahudumu Wote
katika Kituo cha Afya Muriba kwa huduma nzuri na kusema kuwa baadhi ya wagonjwa
wamekuwa wakitoka nje ya wilaya ya Tarime kwa lengo la kwenda kupata matibabu
pale baada ya kuboresha Mazingira.
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Mhe: Moses M. Misiwa aliomba
kamati hiyo kukumbusha Serikali kuleta Fedha za Ruzuku ili kusaidia kusukuma Maendeleo
katika Halmashauri.
“Halmashauri hii ya wilaya ya Tarime inatekeleza miradi yake kwa kutumia
Mapato yake ya ndani tangu 2016 serikali kuu haijawahi kutuletea Ruzuku sasa
kama kamati tunaomba ili suala mulifikishe serikalini” alisema Misiwa.
Aidha Wananchi wamebainisha
Changamoto mbalimbali mbele ya kamati hiyo huku suala la upatikanaji wa maji
safi na salama katika kituo hicho likiibuka,
Comments
Post a Comment