KAMATI YA BUNGE YAPONGEZA UJENZI KITUO CHA AFYA MURIBA.

www.tarimedc.go.tz Kamati ya Bunge ya hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) imepongeza ujenzi wa kituo cha Afya Muriba pamoja na huduma zinazotolewa pale ambapo imeitaka Halmashauri ya wilaya ya Tarime kuendelea kutumia Vyema Mapato yake ya Ndani huku ikitekeleza vyema Miradi ya Maji, Afya , Elimu na Barabara ili kutatu changamoto za Wananchi. Kauli hiyo imetolewa na Mhe: Abdallah Chikota ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo kipindi walipotembelea kituo cha Afya Muriba kwa ajili ya kukagua Miradi hiyo. “Sisi kama Kamati tumejilidhisha pia tunafurahishwa na huduma zinazotolewa hapa na changamoto ambazo zinakumba hiki kituo cha Afya tutaenda kuangalia kwenye vitabu kama zimewekwa ili kuzisemea kwa lengo la kuzitatu” alisema Chikota. Kwa Upande Wake Naibu waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe: Mwita Waitara naye alipongeza Wahudumu Wote katika Kituo cha Afya Muriba kwa huduma nzuri na kusema kuwa baadhi ya wagonjwa wamekuwa wakitoka nje ya wilaya ya Tarime kwa len...